Chelsea imekuwa ikitajwa kumfukuzia mshambuliaji wa klabu ya nchini Italia inayoshiriki ligi kuu nchini umo maarufu kama Serie A, klabu ya As Roma ambaye ni raia wa Bosnia, Edin Dzeko. Imekuwa ikihusishwa kumtaka nyota huyo pamoja na mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo ambaye mwenyewe ni raia wa Italia ingawa ana asili ya Brazil, Emerson Palmeira.
Wakala wa Emerson mwenyewe amekubali kuwa Chelsea inakaribia kumnasa nyota huyo, lakini tabu ipo kwa wakala wa Dzeko anayeitwa Irfan Redzepagic .
Wakala huyo alipohojiwa juu ya Dzeko kutua Chelsea alijibu "Sijui chochote kuhusu hilo mnaloniuliza, sijapata mawasiliano yoyote kuhusu habari hiyo,. Dzeko ni mchezaji halali wa As Roma, nadhani mnalijua hilo. Alafu mbona kila tukizungumza huwa mnaziongelea hizo habari za Chelsea, klabu kutoka China, na za kutoka Mexico. Hizo ni tetesi tu. Ukweli ni kwamba, Dzeko anataka kubaki Roma"
"Je nimewasiliana na Conte? Kwa nafasi yangu siwezi kuwa muwazikwa kila jambo haswa yanayoendelea. Kubwa naloweza kusema Conte anampenda Dzeko, lakini je kuna mtu ambaye hampendi?"
Chelsea imekuwa ikihusishwa kuwa tayari kuoa kiasi cha pesa pamoja na Michy Batshuayi ili wawavute Emerson na Dzeko kutoka klabuni As Roma.

No comments:
Post a Comment