Mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Watford wa jana usiku unaonekana kuzua mengi klabuni Chelsea. Kocha Antonio Conte amekuwa akitajwa kuondoka Che;sea ifikapo mwisho wa msimu huu lakini mara baada ya mchezo huo kukatoka taarifa mpya juu ya kibarua cha kocha huyo akitajwa kuondoka hata kabla ya msimu kuisha. Lakini ukiachana na kocha huyo raia wa Italia, kuna na kiungo Tiemoue Bakayoko ambaye sasa anaonekana kutoimaniwa tena na mashabiki wa Chelsea mara baada ya mchezo huo ambao Chelsea ilipoteza kwa magoli 4-1.
Kutokana na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na nyota huyo, mchambuzi wa soka Ray Wilkins ameibuka na kusema Chelsea ilipoteza ela yake kumsajili mchezaji huyo, na hakukuwa na sababu ya kumsajili nyota huyo raia wa Ufaransa kwa dau kubwa na kumuacha kinda wake Nathaniel Chalobah ajiunge na klabu ya Watford kwa dau la paundi milioni 6
"Chalobah alienda Watford kwa dau la paundi milioni 6 na wakamsajili Bakayoko kwa paundi milioni 40. Wote wakiwa na umri sawa (miaka 23). Ipo wapi tofauti ya paundi milioni 34 kati yao? Mi sioni kama kuna tofauti. Umempata kinda wa kiingereza ambaye umemkuza mwenyewe, na ameshacheza michezo 100 akiwa na timu ya Uingereza, na amelelewa kwenye akademi yako ya Chelsea na anaipenda Chelsea nashangazwa na hichi kilichotendeka nashindwa kuamini" alisema mchambuzi huyo.
Nathaniel Chalobah alikuwa ni kinda na nyota wa Chelsea aliyelelewa
na kukulia klabuni hapo huku akihusika vyema na kuonyesha uwezo mkubwa
huku akitumika kwenye baadhi ya michezo ya Chelsea kabla ya kuuzwa
kwenda klabu hiyo ya Watford ingawa kwa sasa ana majeruhi yanayomfanya
akae nje kwa muda sasa.

BAKAYOKO AZUA MAKUBWA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment