COURTOIS ATOA NENO JUU YA CONTE KUONDOKA CHELSEA - Darajani 1905

COURTOIS ATOA NENO JUU YA CONTE KUONDOKA CHELSEA

Share This
Mara baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, klabu ya Chelsea imekuwa ikihusishwa kuachana na kocha wake Antonio Conte kutokana na mfululizo huo wa matokeo mabovu huku klabu ikishinda michezo miwili tu kati ya michezo 10 iliyocheza mfululizo.

Kumekuwa na makocha kadhaa wakitajwa kuchukua nafasi ya kocha huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kuondoka Chelsea ifikapo mwisho wa msimu huu. Lakini mara baada ya kipigo cha jana kutoka kwa Watford, cha magoli 4-1, ni kama kilitia petroli kwenye moto wa kocha huyo na kufanya kuibuke habari nyingi juu ya kocha huyo kutimuliwa kabla ya muda mfupi uliopita kuripotiwa tena kuwa kocha huyo haondoki Chelsea.

Hapa nakuletea mazungumzo aliyofanyiwa mlinda mlango namba moja wa Chelsea, Thibaut Courtois ambaye ametoa neno juu ya hali ya sasa ilivyo klabuni hapo.

Alipoulizwa juu ya uhusiano wa wachezaji na kocha
"Tunamwamini na tunaiamini timu yetu pia. Tumekuwa na matokeo mawili mabaya na tunajaribu kupambana kurudi katika ubora wetu, kuungana pamoja na kuendelea kupambana. Tulitaka kuonyesha kuwa tunaweza kupambana hata tukiwa wachezaji 10 uwanjani (kwenye mchezo dhidi ya Watford mara baada ya Bakayoko kupewa kadi nyekundu), lakini inakuwa ngumu haswa unapopata matokeo mabovu kama ilivyotokea, haiwezi kuwa rahisi kwetu. Kumeibuka maswali mengi juu yetu lakini muhimu ni kuungana kwa pamoja na kuwa pamoja mazoezini"

"Kiukweli, tumefadhaishwa na matokeo haya tuliyoyapata, kiukweli sio sawa, lakini muhimu ni kusahau na kurudi tena mazoezini na kuweka mambo sawa. Kwa sasa yuna matokeo mawili mabaya, lakini muhimu pia ni kuwa tupo pamoja kama timu, lakini pia tupo pamoja na kocha na kila mmoja analifurahia hilo na tutajitahidi kila iwezavyo kushinda mchezo unaokuja (dhidi ya west Bromwich).

"Kubwa ni kusema, asante kwa mashabiki kwa kuwa wavumilivu na kukubali kuliimba jina la Chelsea hata kwa dakika zote za mchezo, hata tunapokuwa tumepoteza"

Alipoulizwa juu ya penati iliyopatikana katika mchezo dhidi ya Watford
"Deulofeu alikuwa kabla yangu kwenye kuwania mpira nami nilijaribu kujifanya kuwa mdogo kadri nilivyoweza ili nisimguse na nadhani alifanikiwa kudanganya alivyoweza. Kwa upande wangu, haikuwa penati"


Alipoulizwa juu ya mchezo wa jana dhidi ya Watford
"Kipindi cha kwanza  hatukucheza soka safi na kipindi cha pili tulijaribu kupambana tukiwa pungufu na tuliweza kumiliki mpira na kucheza mpira zaidi na tukafanikiwa kupata goli, lilikuwa ni jambo zuri. Lakini ukiangalia kwa goli lao la pili, kama tungejitahidi kumiliki mpira na kujaribu kuwashambulia ingekuwa vyema, ila navyoona tuifanya uzembe na kuwafanya wapate goli la pili ambalo lilikuwa laini sana kwa hivyo ilimaanisha tulikuwa chini ya mchezo. Kwa sasa tunatakiwa kupambana na kujitahidi kurudi kwenye ubora wetu"

No comments:

Post a Comment