MBADALA WA CONTE ATOA TAARIFA MPYA HUKO ITALIA - Darajani 1905

MBADALA WA CONTE ATOA TAARIFA MPYA HUKO ITALIA

Share This
Licha ya jana kutoka taarifa kuwa klabu ya Chelsea haina mpango wa kumtimua kocha wake wa sasa, Antonio Conte ambae amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kuondoka klabuni hapo, anayetajwa kuwa mrithi wa kocha huyo klabuni hapo, Maurizio Sarri inasemekana amekubali kufanya mazungumzo ya kuendelea kubaki kwenye klabu aliyopo kwa sasa, klabu ya Napoli.

Maurizio Sarri ambaye ni kocha wa klabu hiyo ya Napoli inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A, anashika nafasi ya kwanza katika msimamo huo wa ligi kuu huku akiwaacha mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Juventus kwa alama moja amekuwa akihusishwa kutua Chelsea huku mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich inasemekana amekuwa akifanya nae mawasiliano ili amvute Darajani.

Lakini gazeti moja la nchini Italia linadai kuwa kocha huyo anaweza akasaini mkataba mpya klabuni hapo ambapo rais wa klabu hiyo aliahidi kukutana nae ili kufanya nae mazungumzo, na taarifa zinadai ili kocha huyo asaini mkataba mpya klabuni hapo ameandaliwa dau la euro milioni 4 ambalo ni sawa na paundi milioni 3.5 kwa mwaka na inafahamika endapo kocha huyo akisaini mkataba mpya basi lile dau la paundi milioni 7.1 ambalo ni kama dau lake la kuuzwa litafutika.

Inaelezwa kuwa kocha huyo anataka kuendelea kuwepo klabuni Napoli ili kupambania ubingwa wa ligi kuu ambapo kama ataipatia ubingwa msimu huu basi atakuwa ameipa ubingwa mara baada ya ukame wa miaka 28 wa klabu hiyo kushindwa kubeba taji hilo la ligi kuu.

No comments:

Post a Comment