CHELSEA ILIWASHANGAZA WENGI HUKO UINGEREZA - Darajani 1905

CHELSEA ILIWASHANGAZA WENGI HUKO UINGEREZA

Share This
Huenda ulikuwa huijui hii, au hukuwai kuiskia au hata kama uliisikia hukujua kwanibi, nakurudisha nyuma kidogo mpaka msimu uliopita ambapo Chelsea ilifanikiwa kushinda taji la ligi kuu Uingereza ikiwa chini ya kocha Antonio Conte ambapo alikuwa ndio kwanza ameingia kwenye ligi hiyo akitoka kuzifundisha timu kama Juventus na kuiongoza vyema timu ya taifa ya Italia.

Nachotaka nikujuze hapa au kukufahamisha hapa, ni tukio la mchezo wa fainali kati ya Chelsea dhidi ya Arsenyani (Arsenal), mchezo wa fainali ya kombe la FA uliochezwa pale kwenye uwanja wa taifa wa nchi ya Uingereza, Wembley. Wengi walishangazwa siku ile, sio kutokana na Chelsea kupoteza mchezo ila pale wachezaji wa Chelsea walipoingia uwanjani bila kuwa na kitambaa au kishikiza mkono cheusi ambapo ilitakiwa wavae kwa kila mchezaji ili kuonyesha kuhuzunishwa na msiba uliotokea huko jiji la Manchester.

Kabla ya mchezo, klabu ilitangaza na ilifahamika kuwa wachezaji wa pande mbili wote wangetakiwa kuwa na kitambaa au kishikiza mkono hicho ambacho huwa kinavaliwa kwenye mkono karibu na bega na hatimaye wachezaji wote walipoingia uwanjani ikaonekana ni wachezaji wa Arsenyani tu walikuwa wamevaa vishikizo hivyo huku wachezaji wa Chelsea wakiwa hawana kabisa ingawa walisimama kwa heshima kuomboleza kifo hicho au tukio hilo la huzuni kwa dakika moja.

Kipindi cha pili wachezaji wa Chelsea walirudi wakiwa wamevaa vishikizo hivyo ila bado kulitokea mgogoro mkubwa mitandaoni huku wengi wakiishutumu kutokana na tukio lililotokea lilitokea siku tano kabla ya mchezo huo huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kujisahau.

Jambo lile lilizua gumzo mitandaoni na hata wengine kufikia kuikemea Chelsea kuwa hawakuonyesha heshima maana walitakiwa wavae vishikizo hivyo, na mwisho wa siku Chelsea ikapoteza mchezo huo kwa magoli 2-1 huku Victor Moses akipewa kadi nyekundu.

Huenda vile vinyongo vya watu ndivyo vilivyofanya tukapoteza mchezo ule, mmmh! mimi sijui nia yangu ni kukujulisha tu hilo

No comments:

Post a Comment