CHELSEA YAMPATA MBADALA WA CONTE - Darajani 1905

CHELSEA YAMPATA MBADALA WA CONTE

Share This

Klabu ya Chelsea inatajwa kumpata mrithi wa kocha wa sasa, Antonio Conte ambaye anatajwa kuachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu kutokana na kutokuwa na msimu mzuri.

Taarifa zinasema kuwa Chelsea imepanga kumvuta kocha kutoka klabu ya Napoli, Maurizzio Sarri ambaye ni raia wa Italia kama ilivyo kwa kocha Antonio Conte ambapo taarifa zinasema kuwa Chelsea ipo tayari kutoa dau la euro milioni 8 ili kumnyakua kocha huyo ambapo dau hilo ndilo lililoandikwa kwenye mkataba wake kama kuna klabu ikimtaka kumsajili.

Mauirizzio Sarri amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kutua klabuni Chelsea huku pia alikuwa kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa na Chelsea hata kabla ya kuchaguliwa kwa Antonio Conte mwaka 2016 na sasa amekuwa akitajwa kwa muda sasa kuwa anaweza kuwa mrithi wa Conte klabuni hapo huku makocha wengine waliokuwa wanatajwa kuwaniwa na Chelsea wakiwa ni pamoja na Carlo Ancellotti, Luis Enrique, Diego Simeone na Massimiliano Allegri.

No comments:

Post a Comment