Klabu ya Chelsea inahusishwa kumuania nyota wa klabu ya Mama site (Manchester city), Raheem Sterling ambapo mipango hiyo inatajwa kufanyika katika dirisha kubwa la usajili.
Nyota huyo amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Mama site kilichochini ya kocha Pep Guardiola ambapo kwa msimu huu ameshaifungia magoli 14.
Lakini habari zinasema Chelsea itaingia kwenye mbio za kumsajili nyota huyo pale tu Eden Hazard atakaposajiliwa na Real Madrid.
Real Madrid wanatajwa kumuwania kwa karibu Eden Hazard na wameutenga usajili huo wa dirisha kubwa la usajili kama ndio wakati sahihi wa kukamilisha usajili wa nyota huyo raia wa Ubelgiji mwenye miaka 27 kwa sasa.
No comments:
Post a Comment