CONTE AWAJIA JUU WAANDISHI WA HABARI - Darajani 1905

CONTE AWAJIA JUU WAANDISHI WA HABARI

Share This

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amewajia juu waandishi wa habari akiwalalamikia juu ya kukuza mambo kumhusu yeye juu ya kusalia klabuni hapo ambapo kumekuwa na kuzagaa kwa habari juu ya kocha huyo kutaka kuondoka.

"Nashangaa nahusishwa sana na taarifa hizi za kutakiwa kuondoka klabuni hapa, huku wengi wakiwa wanasahau mafanikio tuliyoyapata msimu uliopita huku tukiwa na kikosi dhaifu"

"Kumekuwa na habari zikinihusisha kuondoka. Mimi nina mkataba hapa na nauheshimu, nitaendelea kuwa hapa na nina furaha ya kuwa hapa. Muda wangu ukishaisha sio tutaangalia nini cha kufanya"

"Nina mwaka mmoja na nusu tu hapa, lakini nimekuwa nahusishwa kuondoka" alisema kocha Antonio Conte.

Kumekuwa na taarifa nyingi zikimhusisha kocha Antonio Conte kuondoka klabuni huku kukisambazwa baadhi ya taarifa kuwa hana mahusiano mazuri na baadhi ya makocha wasaidizi.

No comments:

Post a Comment