Chelsea inatajwa kuingia kwenye vita na vigogo wa Ulaya katika mbio za kumsajili mlinzi wa klabu ya Barcelona raia wa Ufaransa, Samuel Umtiti.
Chelsea imeingia kwenye vita hiyo ya kumsajili mlinzi huyo kwenye dirisha kubwa la usajili lijalo huku thamani ya nyota huyo ikitajwa kufikia paundi milioni 60.
Klabu yake ya Barcelona inaangaika kufanya nae mazungumzo ili asaini mkataba mpya ambapo ubaya wa mikataba yao wanaweka kiwango cha kufikia ili kumsajili mchezaji wao na kama ikitokea klabu itakayofikia basi hata kama klabu haitaki kumuuza inalazimika kumuuza kutokana na kufikiwa kiwango kilichopo kwenye mkataba.
Kama Chelsea ikifanikiwa kutoa kiasi hicho cha euro milioni 60 basi itakuwa na asilimia kubwa ya kumnasa huku nyota huyo akitakiwa pia na klabu za Real Madrid, PSG, Manyumbu (Manchester united) na Mama site (Manchester city)
No comments:
Post a Comment