KILICHOJIRI KWA MBADALA WA CONTE - Darajani 1905

KILICHOJIRI KWA MBADALA WA CONTE

Share This

Klabu ya Chelsea imekuwa ikihusishwa kumuwania kwa karibu kocha wa klabu ya Napoli, Maurizio Sarri ambaye amekuwa akitajwa kuwa mrithi au mbadala wa kocha wa sasa, Antonio Conte klabuni Chelsea.

Taarifa zilizogaa zilikuwa zinadai Chelsea ilikuwa inafanya nae mazungumzo kocha huyo ili atue klabuni pale ambapo Antonio Conte ataondoka.

Taarifa zilizotoka zinadai, rais wa klabu hiyo ya Napoli inayoshiriki ligi kuu Italia, Aurelio De Laurentiis anataka kufanya nae mazungumzo ili kumbakisha kocha huyo anayetamba na mtindo wa kampa kampa tena yani ule mtindo wa kutoa pasi unatafuta nafasi kisha unarudishiwa.

"Ninataka kukaa nae chini na kufanya nae mazungumzo ifikapo tarehe 9-Februari (Itakuwa siku ya Alhamisi wiki inayoanza kesho). Ninadhani kubaki kwake itakuwa sahihi maana kuna mipango mingi inataka kufanyika naye atakuwa muhimu kuendelea kubaki. Lakini pia nitatengua dau lake la kusajiliwa la euro milioni 8" alisema rais huyo.

Mkataba wa kocha Maurizio Sarri unakipengele cha dau la kuuzwa, yani kama ilivyo kwa nyota anayetakiwa na Chelsea, Samuel Umtiti naye ana kipengele icho ambapo kama timu ikilifikia dau hilo lililoko kwenye mkataba basi timu yake itake au isitake ni lazima kumuuza na hiyo ndiyo inatajwa kuwepo kwenye mkataba wa kocha huyo.

No comments:

Post a Comment