ENRIQUE AIPA MASHARTI CHELSEA KABLA YA KUTUA - Darajani 1905

ENRIQUE AIPA MASHARTI CHELSEA KABLA YA KUTUA

Share This
Licha ya kuhusishwa kwa muda kidogo juu ya kuwa mrithi wa kocha Antonio Conte klabuni Chelsea, kocha wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa hana timu anayoifundisha, Luis Enrique amekataa kutua Chelsea kwa sasa akitaka kutua hapo mpaka mwishoni mwa msimu.

Kocha Antonio Conte amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo huku Luis Enrique akitajwa na vyanzo vingi kuwa anakaribia kutua klabuni hapo, lakini kocha huyo amekataa kutua klabuni Chelsea katikati ya msimu au wakati msimu unaelekea mwishoni na badala yake anataka kutua mpaka msimu utakapoisha na wakati timu ikiwa inajiandaa na msimu mpya.

Taarifa zilizotoka mwanzo zinadai kuwa kocha huyo ameshakubaliana ahitaji binafsi na Chelsea na kuwa anakaribia kupewa mkataba wa miaka miwili na nusu lakini kwa mahitaji ya kocha huyo kutua kwake Chelsea kutakuwa mara baada ya msimu huu kuisha ili aipange upya timu yake.

Kocha mwengine ambaye anaifundisha klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A, klabu ya Napoli, Maurizio Sarri anatajwa kufanya mazungumzo na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ambapo pia kocha huyo anahusishwa na kutua Chelsea ambapo dau la paundi milioni 7.1 ndilo linatajwa kama dau la kumfanya aondoke klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment