Kumewai kutokea walinzi wengi bora nchini Uingereza na duniani kote ambao ukianza kuwataja haswa waliowai kutokea kwenye miaka ya 2000 mpaka hivi leo, utakuwa haujakamilisha orodha kama utamuacha mfalme wa Chelsea, John Terry ambaye amekuwa na heshima kubwa klabuni hapo mpaka kufikia kuitwa "Legend, Leader, Captain" ikimaanisha Gwiji, Kiongozi, Nahodha ambapo amekuwa akiichezea Chelsea kwa miaka 22 kabla ya kuachana nayo mwishoni mwa msimu uliopita na kujiunga na Aston Villa.
Sasa umemsikia nyota wa klabu ya Everton, Wayne Rooney ambaye amekuwa nyota mkubwa pindi alipoichezea Manyumbu (Man utd)? alichokisema kuhusu John Terry?
Alikuwa mmoja wa wachambuzi katika mchezo wa juzi ambapo Chelsea ilimenyana dhidi ya Watford, na aliulizwa ni mlinzi au beki gani ambaye alipokutana nae aliwai kukiri kuwa ni beki kisiki na mgumu kucheza dhidi yake. Kujibu swali hilo alianza kwa kumtaja Carragher akionyesha kumtania maana walikuwa wote katika uchambuzi siku hiyo, lakini baadae akasema "John Terry, amekuwa mgumu mara zote nilipocheza dhidi yake. kwa miaka sita mpaka saba ambayo nimecheza dhidi yake amekuwa mgumu licha ya kutokuwa na kasi lakini amekuwa akinidhibiti sana"
Je unakumbua lipi kutoka kwa John Terry?

MSIKIE ROONEY ALICHOKISEMA KUMHUSU JOHN TERRY
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment