Mara baada ya kutoka taarifa kuhusu kocha wa Chelsea, Antonio Conte kunusurika kutimuliwa klabuni Chelsea mara baada ya kuiongoza Chelsea kupokea kichapo cha pili mfululizo kwenye ligi kuu Uingereza ikifungwa na Bournemouth kisha na juzi usiku kufungwa na Watford, taarifa mpya tena zimetoka juu ya nafasi ya kocha huyo klabuni hapo ikionekana kuwa matatani.
Gazeti la nchini Hispania linamtaja kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique kuwa mrithi waAntonio Conte klabuni hapo huku ikielezwa kuwa kocha huyo tayari ashafanya makubaliano na Chelsea na kinachosubiriwa kwa sasa ni kuondoka kwa kocha Antonio Conte kisha ndio Enrique atue.
Gazeti hilo linasema kuwa Luis Enriqye amepewa ofa ya miaka miwili na nusu wa kuifundisha Chelsea na huenda usajili huo ukakamilika muda wowote kama Conte ataondoka.

MAPYA YAIBUKA NAFASI YA CONTE KLABUNI CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment