Chelsea inatajwa kumfukuzia kwa karibu nyota raia wa Jamaica, Leon bailey ambaye anaichezea klabu ya Bayer Leverkusen ya nchini Ujerumani inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama Bundesliga.
Leon bailey mwenye miaka 20 anatajwa kwa karibu kutakiwa na Chelsea haswa kocha wa klabu hiyo, Antonio Conte ambaye anamtaja kama chaguo sahihi kutua Chelsea mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo aliwai kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akiwa na jezi za Chelsea ambapo imetafsiriwa kuwa ana mapenzi makubwa na klabu hiyo.
Nyota huyo ametua klabuni hapo miezi 12 iliyopita akitokea klabu inayochezewa na nyota raia wa Tanzania, Mbwana Samatta, klabu ya KRC Genk inayopatikana nchini Ubelgiji ambapo alicheza huko kwa mafanikio makubwa kabla ya kutimkia Bayer Leverkusen.
Kwa sasa ana mkataba klabuni hapo unaoisha mwaka 2022 na amekuwa akihusishwa kutakiwa na Chelsea toka diridha kubwa la usajili lililopita ambapo mpaka sasa ameshaichezea Bayer Leverkusen michezo 18 na kuifuungia magoli nane kwa msimu huu huku akitajwa pia kutakiwa na klabu za Manyumbu (Man utd) na Arsenyani (Arsenal).
CHELSEA YAONGOZA KWA BAILEY
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment