GIROUD ALITUA CHELSEA KISA URUSI - Darajani 1905

GIROUD ALITUA CHELSEA KISA URUSI

Share This

Moja kati ya sajili zilizowashangaza wengi katika dirisha la usajili dogo lililopita la mwezi Januari ni Olivier Giroud kutua Chelsea.

Nyota huyo amefanikiwa kutua Chelsea kwa dau la paundi milioni 18 huku akipewa mkataba wa miezi 18 na kupewa jezi yenye namba 18, hahaaa ni mfuatano wa 18 tu ila kilichowashangaza wengi ni umri wake wa miaka 31 ambapo ni nadra Chelsea kumsajili mchezaji mwenye umri kuzidi miaka 30.

Lakini, ushajua sababu iliyomfanya mshambuliaji huyo atue Chelsea? ipo ivi, mara baada ya kuonekana ni ngumu kwake kupata nafasi katika klabu ya Arsenyani (Arsenal) haswa tu baada ya klabu hiyo kumsajili Pierre Aubameyang basi nyota huyo akaamua kuondoka.

"Nilipata maombi mengi ya kujiunga na klabu kadhaa, Dortmund walinitaka kwa mkopo huku Sevilla na wao wakiniwania lakini nilipopata simu ya Antonio Conte  nikafanya maamuzi ya kutua hapa" alisema Giroud.

"Kocha Deschamps (ni kocha wa timu yake ya taifa ya Ufaransa) aliniambia niondoke Arsenal. Nami kwa kuwa nataka kucheza kombe la dunia ambalo lipo karibuni hapa. Nikaona ni vyema kuondoka" aliongeza nyota huyo.

No comments:

Post a Comment