Kumekuwa kukiripotiwa kuwa na mgogoro klabuni Chelsea, ambapo mgogoro huo unatajwa kumfanya kocha Antonio Conte aonekane hana muda mrefu klabuni hapo huku mwenyewe akikiri anapenda kubaki Chelsea.
Mwandishi wa habari wa ESPN Brazil, Mauro Cezar Pereira amesikika akisema klabuni hapo kuna mgogoro mkubwa na kwamba kwa sasa wachezaji wote wapo dhidi ya kocha wao wakionekana kucheza bila hari wakimsusia timu na hivyo kusababisha kuwepo na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha. Ni Cesar Azpilicueta peke yake aliyebaki upande wa Conte.
Mgogoro mkubwa unaotajwa kuendelea klabuni hapo chanzo kikitajwa kuanzia kwa kuondoka kwa Diego Costa ambaye kuondoka kwake klabuni hapo alitumiwa ujumbe mfupi wa simu na kutaarifiwa kuwa haihitajiki tena na mchezaji huyo kujiunga na Atletico Madrid huku pia ikisemekana kukataa kumuuza nyota huyo kwenda klabu ya China ambapo ingeipatia klabu fungu kubwa la pesa ilisababisha bodi ya Chelsea kuanza kuwa kinyume nae kocha Antonio Conte.
Lakini fukufuku lote hilo likanyamazishwa na ushindi wa dhidi ya Tottenham na ushindi dhidi ya Manyumbu (Manchester united) lakini fukufuku likafumuka tena mara baada ya David Luiz kuonekana hana nafasi tena kwenye kikosi cha kwanza kutokana na nyota huyo kuwa kama kiongozi klabuni hapo.
Kama Chelsea ikipata tena matokeo mabaya kesho basi kuna asilimia kubwa ya kocha huyo kuondoka klabuni hapo lakini pia kama ikifanikiwa kushinda na kupata matokeo mabaya dhidi ya Barcelona katika mchezo wa klabu bingwa ya Ulaya basi kocha huyo atatimuliwa.
Hivyo ndivyo anavyoamini mwandishi huyo, je unakubaliana nae?
No comments:
Post a Comment