Usiku wa leo Chelsea itakuwa uwanja wa Vicarage Road kucheza mchezo wake wa ligi kuu kwa raundi ya 26 ikipambana na wamiliki wa uwanja huo, klabu ya Watford. Mchezo huo ni wa muhimu kwa Chelsea na inatakiwa ipate ushindi ili kujipatia alama tatu muhimu zitakazoifanya ipande kutoka ilipo nafasi ya nne mpaka nafasi ya tatu.
Hapa nakuletea habari muhimu za kuelekea mchezo huo.
Habari muhimu;
Chelsea; Alvaro Morata na Andreas Christensen wataukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa na majeruhi ambapo Morata alipata majeruhi ya mgongo wakati kwa upande wa Christensen alipata majeruhi katika mchezo wa ligi kuu. Huku pia na nyota mpya wa Chelsea, Ross Barkley naye atakuwa majeuhi.
David Luiz na Willian wanaweza wakarudi uwanjani leo kutoka kwenye majeruhi yaliyokuwa yanawakabili huku Olivier Giroud naye anaweza kutumika lakini kwa asilimia chache kuanza kama mshambuliaji namba moja, wakati Emerson nae ni mbadala wa Marcos Alonso kwa hiyo inawezekana kutumika kwake mpaka Marcos apumzishwe.
Watford; Javi Gracia ni kocha mpya klabuni hapo na anakutana na wakati mgumu kutokana na kuwa na nyota wengi majeruhi ikiwemo mlinda mlango wao namba moja, Heurelio Gomes. Lakini pia ikiwakosa na nyota wake kama Tom Cleverley na wengine.
Mwamuzi; Mike Dean atakuwa mwamuzi wa mchezo huu, hii imekuja mara baada ya kubadilisha ambapo mwanzoni ilijulikana kuwa Craig Pawson ndiye atakuwa mwamuzi. Mike Dean atakuwa mwamuzi katika michezo 66 ambayo Chelsea imekuwa uwanjani.
Rekodi; Mara ya mwisho kwa Watford kupata ushindi dhidi ya Chelsea ilikuwa mwaka 1999, toka kipindi icho mpaka leo wameishia kupata sare michezo mitatu huku wakifungwa michezo 10.
Mechi zilizopita;
Chelsea; DWLWL
Watford; WDLLD
Muda; Saa 11:00 Usiku (Saa 23:00) kwa saa za Afrika Mashariki

HABARI MUHIMU KUELEKEA WATFORD vs CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment