MARCOS ALONSO KUCHEZA JUMATATU vs WEST BROM? - Darajani 1905

MARCOS ALONSO KUCHEZA JUMATATU vs WEST BROM?

Share This

Nyota wa Chelsea ambaye ni raia wa Hispania, Marcos Alonso hakuwepo katika mchezo ambao Chelsea ilipoteza dhidi ya Watford ambapo mara baada ya mchezo kocha Antonio Conte alisema aliamua kumpumzisha ili nyota huyo kuwa sawa kutokana na kutumika sana na hivyo kocha kuamua kutokusafiri nae katika kikosi hicho kilichopoteza dhidi ya Watford. Lakini baadhi ya magazeti yalifika mbali na kuripoti kuwa nyota huyo hakuwepo katika mchezo huo kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo ambapo habari hizo hazikutolewa na kocha.

Sasa swali lililopo kwa sasa, je nyota huyo atakuwepo kwenye mchezo wa jumatatu dhidi ya West Bromwich?

Hilo ndilo swali, maana kwa maelezo ya kocha yakusema aliamua kumpumzisha unapata jibu rahisi tu kuwa atakuwepo katika mchezo huo ambao Conte atahitaji apate ushindi ili kujiweka sawa katika msimamo wa ligi kuu ambapo kwa sasa Chelsea inashika nafasi ya tano ikishushwa na Tottenham waliopata ushindi dhidi ya Arsenyani (Arsenal), lakini swali hilo linakuwa gumu endapo maelezo yaliyotolewa na baadhi ya vyanzo kuwa mchezaji huyo alikuwa nje kutokana na kuwa na majeruhi ambapo itakuwa kuna nafasi finyu sana ya muhispania huyo kucheza mchezo huo dhidi ya West Bromwich au maarufu kama The Baggies.

Lakini kwa magazeti ya Times na Guardian yenyewe yametoa taarifa kuwa nyota huyo atakuwepo katika mchezo huo wa raundi ya 27 utakaochezwa Stamford Bridge huku Chelsea ikiwa na kumbukumbu njema ya kupata ushindi mnono dhidi ya klabu hiyo katika mzunguko wa kwanza kwa magoli 4-0. Ambapo magazeti hayo yametabiri kikosi kitakachotumika kwenye mchezo huo huku Marcos Alonso akiwa mmojawapo ikionyesha kuwa kuna nafasi kubwa ya mlinzi huyo wa kushoto anayecheza pia kama winga wa kushoto kutumika katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment