Nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi anayeichezea klabu ya Borrusia Dortmund kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huuu ameifungia tena klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.
Batshuayi ameifungia klabu hiyo goli la kwanza kabla ya baadae Mario Gotze kufunga bao la pili na kuipatia ushindi muhimu klabu hiyo katika mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Hamburg.
Batshuayi alijiunga na wababe hao wa Bundesliga kwa mkopo siku ya mwisho ya dirisha dogo la usajili la mwezi Januari akiruhusiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo mara baada ya Chelsea kukamilisha usajili kwa kumnasa mshambuliaji raia wa Ufaransa, Olivier Giroud.
No comments:
Post a Comment