UMTITI KUTUA CHELSEA, MAPYA YAIBUKA - Darajani 1905

UMTITI KUTUA CHELSEA, MAPYA YAIBUKA

Share This

Chelsea inatajwa kuanza mipango ya mapema ya kukiimarisha kikosi chake ili kujiweka sawa na mipango ya baadae ambapo imekuwa ikihusishwa kuwanasa nyota wenye umri mdogo kutokana na nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza kuonekana kuelekea kuzeeka na kuanza kutoka kwenye soka la ushindani.

Kwa safu ya ulinzi ndiyo inaonekana kuelekea kuwapoteza nyota wake kadhaa ambao ni pamoja na David Luiz, na Gary Cahill ambao wote wana miaka zaidi ya 30 ambapo kwa maana hiyo imeanza kutaka kujiimarisha mapema kwa kuwasajili nyota kadhaa kutoka klabu mbalimbali barani Ulaya.

Moja ya nyota hao ni nyota wa klabu ya nchini Hispania, Barcelona ambapo Chelsea inatajwa kuwa na mpango wa kumsajili mlinzi wa klabu hiyo, Samuel Umtiti ambaye ni raia wa Ufaransa ambapo taarifa zinadai kuwa Chelsea ipo tayari kumpa mshahara zaidi na anaolipwa klabuni Barcelona ambao ni dau la euro milioni 3 kwa mwaka.

Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde alipohojiwa juu ya usajili na tetesi zinazoenea kuhusu mchezaji huyo alisema "Umtiti ni mchezaji muhimu kwa Barcelona, na tayari mazungumzo yameshaanza na huenda akasaini mkataba mpya na tukaendelea kuwa nae hapa"

Lakini kuna fununu za kuaminika kuwa nyota huyo hataki kuendelea kucheza Hispania ambapo ndoto zake ni kutua Uingereza, kwa fununu hizo zinaifanya Chelsea kuwa na nguvu katika mpango wake wa kumnasa mlinzi huyo ingawa itapata upinzani kutoka kwa klabu ya Manyumbu (Man utd) ambao wao wanatajwa kumtaka pia mfaransa huyo.

Ili Chelsea imnase mchezaji huyo mwenye miaka 24 kwa sasa, italazimika Chelsea itoe dau la paundi milioni 54 ili kumnasa nyota huyo.

No comments:

Post a Comment