Chelsea itashuka uwanjani katika mchezo wake unaofata dhidi ya Tottenham, ambapo Chelsea itakuwa nyumbani Stamford Bridge kucheza mchezo huo wa ligi kuu Uingereza.
Kuelekea kwenye mchezo huo kulikuwa na taarifa za kuhuzunisha juu ya wachezaji wa Chelsea ambao waliripotiwa kuwa na majeraha na hivyo kurudishwa kutoka kwenye timu zao za taifa na kurejea Chelsea ili kujiweka sawa.
Moja kati ya wachezaji hao, alikuwa ni mlinda mlango nambari moja wa Chelsea, Thibaut Courtois ambaye majeraha aliyoyapata kabla ya mchezo uliopita Chelsea ilipopata ushindi dhidi ya Leicester katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la FA ameonekana kutokuwa sawa kuweza kutimiza majukumu yake kwa timu ya taifa na hivyo kurudishwa klabuni Chelsea ili kuwekwa sawa kitabibu.
Kocha wake wa timu ya taifa, Roberto Martinez amesema timu yake imelazimika kumruhusu nyota huyo kurejea klabuni Chelsea ili ajiweke sawa na anatazamia nyota huyo kuwa sawa mpaka kufikia mwisho wa wiki hii na hivyo kuwepo uwezekano wa kucheza katika mchezo wa Chelsea dhidi ya Tottenham.
No comments:
Post a Comment