Chelsea imepata ushindi wake muhimu hapo jana, ushindi unaoipleka hatua ya nusu fainali ya kombe la FA ambapo mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Wembley dhidi ya Southampton ambayo inafundishwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Mark Hughes.
Lakini wiki hii hakutakuwa na michezo ya ligi wala michezo inayohusisha klabu kupambana na badala yake kutachezeka michezo ya kimataifa ambapo wachezaji kadhaa waliochaguliwa na makocha wa timu zao za taifa watajiunga na timu hizo katika wiki hiyo ya michezo ya kimataifa ambapo mchezo uliombele ya Chelsea ni dhidi ya Tottenham, mchezo utakaochezwa tarehe 1-Aprili.
Lakini kutokana na ushindi ambao Chelsea ilipata jana na kutokana na kusimama kwa michezo ya vilabu na kupishwa michezo ya timu za taifa nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye ataungana na timu yake ya taifa ya Ubelgiji ametuma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter akifurahia ushindi wa Chelsea katika mchezo wa jana, lakini akionyesha kujiandaa vyema ili kutimiza majukumu yake katika timu ya taifa.
"Ninafuraha kutokana na ushindi, ni upambanaji mzuri vijana wangu, tunaelekea Wembley! Sasa ni mudawa kujiandaa ili kuungana na timu ya taifa #redtogether #chelseafc"
EDEN HAZARD ATOA NENO MARA BAADA YA MCHEZO DHIDI YA Leicester
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment