Heri ya kuzaliwa Fernando Torres - Darajani 1905

Heri ya kuzaliwa Fernando Torres

Share This
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nyota wa zamani wa Chelsea, Fernando Torres ambaye alizaliwa tarehe kama ya leo miaka 34 iliyopita, nasi kama mashabiki wa Chelsea hatuwezi kuruhusu siku hii ipite bila kutoa pongezi kwa nyota huyo japo kwa sasa anaichezea klabu ya atletico Madrid nchini Hispania.

Hongera zako nyota wa kihispania uliyeihakikishia Chelsea kucheza fainali katika mchezo dhidi ya Barcelona mwaka 2012 kwa goli lako la dakika za majeruhi na kufanya Chelsea ifudhu kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-3.

Nyota huyo alionekana kuisha makali yake tangu alipotua klabuni Chelsea akitokea klabu ya Liverpool huku akisajiliwa kwa dau lililovunja rekodi ya usajili kwa miaka hiyo ambapo Chelsea ilimnasa kwa paundi milioni 50.

Lakini je unajua kama ukame wake wa magoli ulikuwa na baraka nyingi kwake? Ndiyo baraka maana hakuifungia Chelsea magoli mengi lakini alishinda mataji mengi akiwa Chelsea kuliko hata alivyokuwa na makali yake klabuni Liverpool, na ndio maana alipofanikiwa kushinda taji la kwanza la klabu bingwa barani Ulaya akiwa klabuni Chelsea mwaka huohuo wa 2012 alitoa ujumbe uliosema "Nimefunga magoli Liverpool lakini nimekuja kushinda mataji Chelsea".

Na kama haujui toka alipocheza Liverpool kwa miaka minne yaani toka mwaka 2007 mpaka mwaka 2011 hajafanikiwa kushinda taji lolote klabuni hapo, lakini alipotua Chelsea mwaka 2011 alifanikiwa kushinda mataji matatu yaani klabu bingwa Ulaya mwaka 2012, kombe la FA mwaka huohuo na taji la ligi ya Europa mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment