Nyota wa Chelsea ambaye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu UIngereza msimu uliopita, N'golo Kante ametoa neno mara baada ya kuhusishwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya PSG ambayo ina nia ya kumnasa nyota huyo ili kuziba pengo la kiungo wake, Thiago Motta ambaye umri wake unamtupa mkono katika soka la ushindani.
"Chelsea ni nyumbani, najihisi kuwa nyumbani nikiwa hapa. Na kwa sasa mimi ni mchezaji wa Chelsea. Nina miaka miwili tu toka niwe hapa, msimu uliopita ulikuwa mzuri kwetu. Nimekuwa hapa na tumefanikiwa kuheza klabu bingwa Ulaya, na naamini tunaenda kumaliza katika klabu nne zajuu na msimu ujao tucheza tena" alisema kiungo huyo ambaye ni raia wa Ufaransa.
Nyota huyo ambaye amekuwa mchezaji bora katika mchezo uliopita ambapo Chelsea iliibamiza Leicester katika mchezo wa robo fainali na kufanikiwakufudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa viungo bora barani Ulaya. Nyota huyo ana mkataba na Chelsea unaoisha mwaka 2021.
Kante atoa neno kuhusishwa kuondoka kwake Chelsea
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment