Chelsea inafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali na kufanikiwa kufika nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo mara baada ya usiku wa leo kupata ushindi wa magoli 1-2 dhidi ya Leicester city iliyokuwa nyumbani na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.
Chelsea ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa nyota wake raia wa Hispania, Alvaro Morata akipokea pasi safi kutoka kwa Willian aliyekokota mpira huo kutokea upande wa Chelsea. Morata anaifungia Chelsea goli hilo likiwa ni goli lake la 11 toka afike Chelsea na linakuwa goli lake la kwanza kwa mwaka 2018 mara baada ya nyota huyo kukumbwa na upepo mbaya na kumfanya kutokuwa na bahati ya goli. Lakini nikuchekeshe kitu, unajua kama kocha Antonio Conte alitabiri kama Morata atafunga. Siku ya ijumaa wakati kocha Antonio Conte alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari, aliuliza juu ya kwanini Morata na Gary Cahill hawajaitwa kwenye timu zao za taifa, kocha Antonio Conte alitoa maelezo marefu lakini alipofika juu ya ubora wa Morata kushuka kisa kutokufunga kwa muda mrefu alisema "....naamini ni mchezaji, na inawezekana jumapili hii (vs Leicester) anaweza akafunga...." na kweli leo Morata amefunga goli safi kabisa na kuifanya Chelsea iwe mbele mpaka mpira kwenda mapumziko.
Kipindi cha pili, kilikuwa kigumu pande zote ingawa Chelsea ilionekana kuruhusu kushambuliwa zaidi mpaka pale Riyad Mahrez alipotumbukiza kwenye eneo la hatari la Chelsea na kuwafanya kutokee kubabatizana kati ya walinzi wa Chelsea na wachezaji wa Leicester mpaka pale mshambuliaji wao Jamie Vardy alipofunga na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka mpira unaisha.
Wakati mashabiki wengi haswa wa huku kwetu wakizani sasa ni mchezo wa marudiano wakizoea kama ile sheria ya nacheza kwenu, tukitoka suluhu unakuja kwetu basi hii ya leo ilikuwa tofauti maana ilihitajika lazima ziongezwe dakika 30 mpaka mshindi apatikane.
Timu zikajiandaa kwa pande zote mbili, na mpira ukaanzishwa kwa nyongeza za dakika 30, 15 za kipindi cha kwanza na 15 za kipindi cha pili.
Willian akatoka, huku nafasi yake ikichukuliwa na Pedro ambaye mabadiliko yake yalizaa matunda mara baada ya kiungo wa Chelsea, N'golo Kante kutoa pasi murua iliyomfikia vilivyo Pedro ambaye hakufanya makosa akitumia kichwa chake kufunga goli tamu lililoifanya Chelsea kutinga hatua ya nusu fainali.
No comments:
Post a Comment