Gwiji wa soka raia wa Uingereza ambaye ni mkongwe na nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry ambaye kwa sasa ni mchezaji na nahodha wa klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza (Championship) ametumia mtandao wa Instagram kutuma ujumbe kwa mlinzi wa kushoto wa Chelsea, Marcos Alonso ambaye ni raia wa Hispania kwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji waliochaguliwa kwenye timu ya taifa ya Hispania.
Mkongwe huyo ametuma picha ya nyota huyo akiwa pamoja na baba yake Marcos Alonso Inaz pamoja na mzee Marcos Alonso Pena ambaye ni babu yake na nyota huyo ambao wote waliwai kuwa wachezaji kwa miaka hiyo huku wote wakiichezea timu ya taifa ya Hispania na mkongwe John Terry akiandika maneno ya kumpongeza nyota huyo kwa kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachocheza michezo ya kirafiki inayotambulika na FIFA mwishoni mwa mwezi lakini pia kwa kufuata nyayo za babu pamoja na baba yake.
Nasi kama Darajani 1905, tunachukua fursa hii kumpongeza nyota huyo kwa nafasi hiyo kubwa aliyoipata.
No comments:
Post a Comment