Nyota wa Chelsea, Ethan Ampadu ambaye kwa sasa ana miaka 17, ametupwa nje ya kikosi cha Wales mara baada ya kuonekana majeraha aliyokuwa nayo yataendelea kumweka nje.
Nyota huyo ametupwa nje ya kikosi cha timu ya taifa ya Wales mara baada ya kuteuliwa hapo kabla kuungana na kikosi hicho kwenye michezo ya kirafiki ya kimataifa inayotambulika na shirika la soka duniani maarufu kama FIFA lakini baadae jina lake likatenguliwa kwenye timu hiyo mara baada ya kuonekana majeruhi aliyoyapata kwenye ushindi wa Chelsea katika michuano ya klabu bingwa kwa vijana maarufu kama UEFA Youth dhidi ya Real Madrid kumfanya kuwa nje zaidi.
Ethan Ampadu aliiongoza Chelsea kwenye mchezo huo uliochezwa siku ya jumatano huku nchini Hispania, mchezo ambao Chelsea ilipata ushindi wa mabao 2-4 dhidi ya Real Madrid na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali dhidi ya FC Porto ambapo kwenye mchezo huo, Ampadu alipata majeraha yaliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo ambapo majeraha hayo yameonekana kuwa makubwa na kuwafanya viongozi wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Wales kuliengua jina lake.
Ugua pole Ampadu.
No comments:
Post a Comment