Nyota huyo ametoa majibu juu ya tetesi hizo na kipi anakiwaza kwa sasa juu ya hatma yake klabuni hapo ambapo mkataba wake wa sasa unaisha msimu ujao.
"kwa sasa nipo Chelsea. Nina mkataba hapa mpaka mwaka ujao na nitaendelea kuwa hapa. Na nitajitahidi kuwa bora zaidi"
"Ni kweli mpaka sasa sijasaini mkataba mpya lakini nafikiri huu sio muda sahihi wa kulifanya hilo. Nahisi itakuwa vizuri kama nikafanya hivyo mpaka msimu ukiisha. Jambo kubwa naloweza kusema ni kwamba, kwa sasa ninafikiria kuhusu Chelsea lakini pia kuhusu mwaka ujao"
"Sina jambo jengine la kusema. Ni rahisi unapokuwa na mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wako watu wakaanza kuongea kuhusu mambo fulani. Lakini kwa upande wangu nazani jambo muhimu kwa sasa ni kufikiria kuhusu kushinda michezo ya ligi iliyobaki na kupambana ili kuingia kwenye klabu nne za juu na kufudhu kucheza klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao, lakini pia kushinda kombe la FA" alisema nyota huyo

No comments:
Post a Comment