HABARI MUHIMU KUELEKEA Leicester vs CHELSEA - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA Leicester vs CHELSEA

Share This

Mara baada ya kushindwa kuendelea kwenye hatua inayofata ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, Chelsea leo itakuwa ugenini ili kupambania nafasi yake nyengine ya kuendelea katika hatua ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Leicester city katika uwanja wa King Power.

Kama ilivyoada, kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu za kuuhusu mchezo huo na kihistoria kwa ufupi.

Habari Muhimu;
Chelsea; Kuelekea kwenye mchezo huu, Chelsea itashuka uwanjani ili kupambana kushinda mchezo huu na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua inayofata ambayo ni hatua ya nusu fainali, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa la Uingereza, Wembley. Inaaminika kocha Antonio Conte analitazama kombe hili kama nafasi pekee kwa Chelsea ili kushinda taji msimu huu kwa maana hiyo inaonekana atakitumia kikosi chake cha kwanza ili kupambana katika mchezo wa leo..

Wachezaji wanaotajwa kuwa majeruhi ni David Luiz pamoja na Ross Barkley wakati kwa upande wa Tiemoue Bakayoko anaweza kutumika kwenye mchezo wa leo mara baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Leicester city; kwa upande wa klabu hii iliyochini ya kocha wa zamani wa timu aliyowai kupita nyota wa Chelsea, Eden Hazard, klabu ya Lille, mzee Claude Puel inatazamia kuwakosa nyota wake Amartey pamoja na Robert Huth ambao wote wanatajwa kuwa majeruhi.

Michezo iliyopita;
Chelsea; DLLWL
Leicester; LWDDW

Rekodi; Katika michezo mitano ambayo Chelsea imecheza dhidi ya Leicester katika hatua ya mtoano, Chelsea imepata ushindi kwenye michezo yote.

Muda; Saa 7:30 Usiku (Saa 19:30) Kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment