Nyota wa Chelsea, Marcos Alonso leo anaweza akaitumikia kwa mara ya kwanza timu yake ya taifa ya Hispania itakapokuwa uwanjani kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo wa kirafiki unaotambulika na chama cha soka duniani (FIFA).
Nyota huyo amekuwa na misimu mizuri tangu alipofika klabuni Chelsea mwaka 2016 akitokea klabu ya Fiorentina ya nchini Italia na mpaka sasa amefanikiwa kujitambulisha vyema na kukuza vyema jina lake akitajwa kuwa mmoja wa walinzi wa kushoto wenye kiwango bora kwa sasa amekuwa akihusishwa kutakiwa na klabu ya nchini Hispania, Real Madrid.
Nyota huyo ametoa majibu juu ya tetesi hizo akisema kwa sasa anaitazamia Chelsea na kuangalia kwa kiasi gani anaweza kuisaidia klabu yake ifikie mafanikio ambayo inapanga kuyafikia.
Real Madrid imetajwa kuwa tayari kumsaka nyota huyo mwenye uwezo mkubwa katika safu ya ushambuliaji japo kiasili ni mlinzi wa kushoto.
No comments:
Post a Comment