Chelsea inajiandaa kushuka uwanjani kumenyana dhidi ya Tottenham kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa raundi ya 31 huku Chelsea ikihitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo unaochezwa jumapili ili iweze kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha Antonio Conte leo amefanya mkutano na waandishi wa habari na kuhojiwa mengi yaliyoendelea na yanayoendelea klabuni hapo. Moja kati ya mambo aliyoyatolea majibu ni pamoja la wachezaji majeruhi wenye hatihati ya kucheza mchezo huo. Kocha huyo akatoa majibu kwa kusema David Luiz na Andreas Christensen wote wana hatihati ya kucheza mchezo huo huku kwa nafasi ya ulinzi wa kati akitegemewa kutumika Gary Cahill ambaye mara nyingi amekuwa akitumika kama mlinzi wa kati anayecheza pembeni.
Ross Barkley na Ethan Ampadu wote wataukosa mchezo huo ambapo kwa upande wa Ampadu anaweza kuwa nje mpaka msimu kuisha lakini pia kwa Courtois ambaye alirudishwa kutoka timu ya taifa na kurudi Chelsea kutokana na majeraha anaaminika kuwa sawa na kutumika siku hiyo.
No comments:
Post a Comment