Nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi anayeichezea klabu ya Borrusia Dortmund kwa mkopo amefanikiwa kushinda tunzo yake ya kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.
Nyota huyo amechaguliwa kuwa mfungaji wa goli bora la mwezi Marchi alilolifunga kwenye mchezo wa ligi kuu Ujerumani kati ya Dortmund dhidi ya Hannover.
Mchezo huo uliochezwa tarehe 18-Marchi uliisha kwa goli 1-0, goli likifungwa na Batshuayi ambapo goli hilo ndilo lililoshinda kuwa goli bora la mwezi Marchi ambapo alilifunga akionganisha krosi safi iliyopigwa kwa mpira wa kona uliopigwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Andre Schurrle na nyota huyo kuonganisha kona hiyo kwa kupiga mpira uliopigwa kiustadi wa hali ya juu.
Nyota huyo amekuwa na msimu mzuri tangu ajiunge na klabu hiyo ambapo mpaka sasa ameshaichezea michezo 13 huku akiifungia magoli tisa na kutengeneza moja, hiyo ni kwa michuano yote.
No comments:
Post a Comment