Klabu ya Chelsea ilihusishwa kwa karibu kumfukuzia winga raia wa Jamaica anayeichezea klabu ya nchini Ujerumani inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama Bundesliga.
Leon Bailey ambaye anatajwa kuwepo pia kwenye mipango ya klabu ya Bayern Munich ambayo nayo inatamani saini ya nyota huyo ingawa haionekani kama Leverskusen watakubali kumuuza nyota wao kwa wapinzani wao na hivyo kuipa nafasi kubwa Chelsea kumnasa winga huyo.
Kwa taarifa zilizopo zidai Chelsea ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 70 ili kumnasa nyota huyo ambaye ameichezea klabu hiyo michezo 30 na kuifungia magoli 9.
Lakini pia nyota huyo alituma picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha akiwa jijini London ambapo picha hiyo ilizidisha tetesi za kuonyesha kuna uwezekano mkubwa kwa Chelsea kuinasa saini ya mjamaika huyo.
No comments:
Post a Comment