Giroud aizima rekodi ya gwiji wa Ufaransa, na habari nyengine soma hapa - Darajani 1905

Giroud aizima rekodi ya gwiji wa Ufaransa, na habari nyengine soma hapa

Share This

Siku ya jana kulichezwa michezo ya kirafiki kwa timu za taifa ambapo timu zilizofudhu kucheza kombe la dunia walikuwa wakivitumia vikosi vya wachezaji wao waliowateua kucheza kombe la dunia ili kujiandaa na michuano hiyo. Hapa nakuletea baadhi ya wachezaji wa Chelsea na timu zao za taifa zilizoshuka uwanjani hapo jana.

Nyota na mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud jana aliiongoza timu yake ya taifa ya Ufaransa kuibamiza magoli 2-0 timu ya taifa ya Ireland.

Giroud aliifungia goli moja katika mchezo huo wa kujiandaa na michuano ya kombe la dunia litakaloanza baada ya siku 15 zijazo. Katika mchezo huo nyota mwenzake klabuni Chelsea, N'Golo Kante hakufanikiwa kupata nafasi ya kucheza huku akiwa kwenye benchi.

Kwa goli hilo linamfanya Zidane kufikia rekodi ya ufungaji wa muda wote kwa upande wa timu ya taifa ya Ufaransa kwa muda wote ambapo amefanikiwa kufikia magoli 31 sawa na magoli yaliyofungwa na gwiji huyo ambaye kwa sasa ni kocha wa Real Madrid. Bado ana kazi ya kupambania kuvunja rekodi za ufungaji kwa magwiji wengine kama Trezeguet pamoja na Thierry Henry kwenye timu hiyo.

Nyota mwengine wa Chelsea, Victor Moses ambaye ni raia wa Nigeria hakupewa nafasi ya kucheza kwenye mchezo mwengine wa kujiandaa na michuano mengine hapo jana wakati timu yake ya taifa ya Nigeria ilipotoka sare na timu ya taifa ya DRC Congo kwa magoli 1-1 huku nyota wengine wa Chelsea, Ola Aina na Omeruo wakipata nafasi ya kucheza mchezo huo wakiingia kama wachezaji wa akiba.

Davide Zappacosta naye aliiongoza vyema timu yake ya taifa ya Italia iliyokua chini ya kocha Roberto Mancini akiifundisha kwa mara ya kwanza tangu atangazwe kuwa kocha wa timu hiyo ambapo aliiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa kirafiki kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Saudi Arabia.

Nyota mwengine wa Chelsea atakayekua mchezo usiku wa leo ni pamoja na Willy Caballero ambaye ataiongoza timu yake ya taifa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nicaragua.

No comments:

Post a Comment