Mmiliki wa Chelseea aweka rekodi Israel - Darajani 1905

Mmiliki wa Chelseea aweka rekodi Israel

Share This

Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amekamilisha vigezo na kukabidhiwa rasmi kibali cha kuishi nchini Israel kwa mkataba wa miaka kumi na kuweka rekodi mpya nchini humo kwa kuwa mtu mwenye utajiri zaidi nchini Israel.

Abramovich mwenye utajiri unaotajwa kufikia paundi bilioni 9 alifika kwenye ubalozi wa Israel uliopo nchini Urusi kwenye juji la Moscow na kukubaliwa ombi lake la kupewa kibali cha kuishi nchini Israel ambapo hii inazidisha fununu za mmiliki huyo kuwa na mpango wa kuiuza klabu ya Chelsea.

Abramovich ambaye alimaliza miaka iliyopo kwenye kibali chake cha kuishi nchini Uingereza toka mwezi Aprili mwaka huu huku akishindwa kuhudhuria fainali ya kombe la FA wakati Chelsea ilipotwaa taji hilo kwa kuibamiza goli 1-0 klabu ya Manchester united.

Kwa taarifa zilizopo zinadai Abramovich alishajaribu kuomba kibali kipya cha kuishi nchini Uingereza lakini kutokana na kutokua na maelewano mazuri kati ya nchi yake ya Urusi pamoja na nchi ya Uingereza basi kumekua na sintofahamu juu ya kukipata kibali hicho na hivyo kuamua kutimkia nchini Israel, nchi ambayo amekua akiitembelea mara kadhaa mpaka alifanikiwa kujenga hoteli nchini humo mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment