Klabu zinazoshiriki ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga, klabu za Valencia na Villareal zinatajwa kufukuzia saini ya nyota na kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas.
Klabu hizo kwa pamoja zinagombania saini ya kiungo huyo raia wa Hispania ambaye mpaka sasa ameshaiongoza Chelsea kushinda mataji manne toka afike klabuni hapo, mataji mawili ya ligi kuu, taji moja la kombe la FA na kombe la ligi.
Fabregas mwenye miaka 31 aliwai kukaririwa akisema ana furaha ya kusalia klabuni Chelsea huku akifurahia maisha ya jiji la London aliyoanza kuyaishi tangu akiwa Arsenal kabla ya baadae kurejea Barcelona na Mourinho kumsajili tena kutua Chelsea.
Nyota huyo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na huenda Chelsea ikakubali kumuuza katika dirisha hili kubwa ama dirisha dogo la mwezi Januari ili asiondoke bure pale mkataba wake utakapoisha.
No comments:
Post a Comment