Kocha wa zamani wa klabu ya Napoli, Maurizio Sarri ambaye kwa sasa anafukuziwa kwa karibu na Chelsea inayotafuta kocha wa kurithi nafasi ya kocha wa sasa klabuni hapo anayetajwa kukaribia kuachana na klabu hiyo ambapo ameifundisha kwa misimu miwili tu huku akiisaidia kushinda mataji mawili.
Kocha huyo anatajwa kukamilisha mazungumzo ya mahitaji yake binafsi na kuna uwezekano wa muda wowote kutambulishwa kuwa kocha mpya wa Chelsea.
Nyota wa klabu ya Napoli, Lorenzo Insigne ambaye amefundishwa na kocha huyo amezungumza juu ya kocha huyo kuondoka klabuni hapo lakini akizua gumzo mara baada ya kutoa kauli iliyotafsiriwa kuwa kocha huyo anamalizia mipango ya kutua Chelsea.
"Kwa kuwa Sarri ni kocha wa Chelsea basi nakubali ata kuungana nae ata nikienda kukaa benchi na kuwa mchezaji wa akiba" alisema nyota huyo akionyesha mapenzi yake kwa kocha wake huyo ambaye rasmi hatoendelea kuifundisha Napoli kwa msimu mwengine haswa kutokana na klabu yake kumtangaza Carlo Ancelotti kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.
Insigne ni moja ya wachezaji nyota klabuni Napoli ambapo gwiji wa soka klabuni hapo, Diego Maradona ambaye namba 10 ya jezi aliyokua akiivaa ilitengwa kutokuvaliwa na mchezaji yoyote toka gwiji huyo kupita klabuni hapo lakini Maradona alitokea kupendezwa na ubora wa Insigne mpaka kuruhusu mchezaji huyo ndiye anastahili kuvaa namba 10 kwa klabu ya Napoli. Insigne anayecheza kama kiungo mshambuliaji mwenye miaka 26 ameichezea Napoli michezo 47 huku akiifungia magoli 14 na kutengeneza mengine 11.
No comments:
Post a Comment