Chelsea bado haionekani kutamani kusalia na kocha wake aliyeisaidia klabu hiyo kushinda mataji mawili kwenye misimu miwili ya kuwa klabuni hapo, Antonio Conte. Taarifa zinadai klabu hiyo inamtazamia kocha wa zamani wa Napoli, Maurizio Sarri kuwa mrithi wa muitaliano mwenzake klabuni hapo.
Lakini kocha mwenzao ambaye naye ni raia wa Italia ambaye aliwai kuifundisha Chelsea kabla ya kutimuliwa mwaka 2004, Claudio Ranieri amemtetea Maurizio Sarri kama je ataweza kuipa mafanikio Chelsea wakati kwenye miaka yake 13 ya ukocha hajawai kutwaa au kuisaidia timu yoyote kutwaa taji lolote? je ataweza kufikia mafanikio aliyoyafikia Antonio Conte kwa misimu miwili kutwaa mataji mawili?
Ranieri alisema "Nadhani ye ni kocha bora, na anaweza kufanya makubwa. Na sio kama hajawai kufanya makubwa maana alipotoka Empoli na kutua Napoli alifanya makubwa mpaka kutambulika na dunia nzima." alisema kocha huyo ambaye aliwai kuisaidia Leicester kutwaa taji lake pekee la ligi kuu Uingereza.
Maurizio Sarri anatajwa kukaribia kusaini klabuni Chelsea mara baada ya wawakilishi wake kufikia makubaliano binafsi na uongozi wa Chelsea ili kumsajili kocha huyo mwenye miaka 59.
No comments:
Post a Comment