Huenda dirisha hili kubwa la usajili likawa dirisha litakalowashuhudia nyota wengi kutoka ligi kuu ya Italia haswa kwa klabu ya Napoli wakatua Chelsea. Ujue kwanini? kuna orodha ya nyota kibao kutoka klabuni hapo wapo tayari kuhama na kocha wao wa zamani, Maurizio Sarri ambaye anatajwa kukaribia kutua Chelsea.
Kocha huyo tayari ameshawataja wachezaji wanne ambao anahitaji kuungana nao klabuni Chelsea endapo usajili wake utakamilika, kuwasoma wachezaji hao, bonyeza hapa na tayari nyota mwengine anayejulikana kama Lorenzo Insigne tayari ameshasema yupo tayari kutua Chelsea kama Sarri akikamilisha usajili wa kutua Chelsea. Na sasa kuna mwengine ameeleza anatamani kutua Chelsea.
Unamjua ni nani? ni kiungo raia wa Italia, Jorginho ambaye kupitia kauli ya wakala wake anatajwa kupendezwa na Chelsea kumtamani nyota huyo ingawa haijafanya mawasiliano yoyote.
Wakala huyo amesema "Manchester city ndio wanamtaka Jorginho lakini hilo nadhani angepaswa kulijibu kiongozi wa Napoli, Guintoli."
"Sina mamlaka ya kuzungumzia juu ya hili kwa sababu sielewi lolote juu ya usajili huu. Chelsea haijafanya mawasiliano yoyote nami kwa hiyo siwezi kuwaongelea pia, hawajaniita ili tufanye mazungumzo."
"Wao (Chelsea) ni timu bora na inavutia kama ilivyo kwa Barcelona na Real Madrid lakini hawajafanya mazungumzo yoyote namimi" alisema wakala huyo anayeitwa Santos Silva ambapo alikua akifanya mahojiano na chombo cha habari cha Calcio Napoli.
Kwa kauli hiyo inaonyesha kwa kiasi gani Chelsea itakuwa na nafasi nzuri ya kuwanasa nyota kutoka Napoli haswa endapo itafanikiwa kumnasa kocha Sarri mwenye miaka 59 ambapo kocha huyo anatajwa kuwa na sifa ya kuwa karibu na wachezaji anaowafundisha hali inayomfanya kupatana nao.
No comments:
Post a Comment