Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika kuinoa kwake Chelsea lakini haionekani kama ataendelea kuifundisha klabu hiyo haswa kutokana na mgogoro uliopo kati yake na viongozi wa klabu hiyo lakini pia kwa kushindwa kuisaidia klabu hiyo kumaliza kwenye klabu nne za juu katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza na hivyo kushindwa kufudhu kucheza klabu bingwa msimu ujao.
Tayari Chelsea inatajwa kumfukuzia kocha wa zamani wa Napoli, Maurizzio Sarri ambaye kwa sasa ameachana na klabu hiyo wiki iliyopita huku kocha mwenzake raia wa Italia, Carlo Ancelotti akichukua mikoba ya kocha huyo kwenye klabu hiyo ya Italia.
Kocha wa klabu ya Manchester city, Pep Guardiola ametoa neno kuhusu Sarri kutua Chelsea ambapo amesema "Sarri ni moja kati ya makocha bora."
"Wengi wetu tunatazama mafanikio ya kocha kwa mataji aliyoshinda, ni kweli hakuna taji aliloshinda lakini ukiizungumzia Napoli ni moja ya klabu iliyocheza soka safi kwa msimu huu. Natamani atue mapema ili nicheze dhidi yake." alisema kocha huyo alipohojiwa na chombo cha habari cha RMC.
Chelsea inatajwa kuwa tayari kutoa kiasi cha euro milioni 4 ili kumnasa kocha huyo mwenye miaka 59 wakati Napoli wanataka euro milioni 8 ambalo ndilo dau lililoko kwenye mkataba wa kocha huyo.
No comments:
Post a Comment