Siku ya leo kumefanyika michezo maalumu iliyoandaliwa na uongozi wa klabu za Chelsea ikiwaleta karibu wale watoto na vijana wote wenye mapungufu kupitia mpango wake wa Chelsea Foundation ambapo klabu ya vijana wenye umri chini ya miaka 12 ya Chelsea imebeba kombe hilo la michezo hiyo ya bonanza kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Klabu ya Chelsea ilianzisha mpango wa kuisaidia jamii kwa nyanja tofautitofauti kwa kuwaleta karibu wale wasiojiweza au wenye mahitaji maalumu kupitia michezo haswa mchezo wa soka ambapo wachezaji wa timu mbalimbali kupitia klabu mbalimbali walishiriki michezo hiyo iliyowaleta kwa pamoja na kufurahi pamoja.
Hii ni moja ya ndoto ambayo blog hii ya Darajani 1905 inatamani itimie kupitia kampeni yake ya Charity For The Blues ambayo ilianzishwa maalumu ili kuifanya jamii haswa ya Afrika ifaidike kwa mapenzi yetu kwa mchezo wa soka lakini haswa kwa kuipenda kwako Chelsea.
Je unahitaji kuungana nasi kwenye kampeni hii ambayo itakuwa inaandaa dhiara na shughuli mbalimbali kama kujitolea kwa jamii ili ifaidike na kile tunachokipenda kama mashabiki? basi unaweza kutuma maombi yako au kupata mawasiliano zaidi juu ya kampeni hii kupitia namba ya simu +255629964908 au email yako kwetu kupitia eng.bakayoko@gmail.com
No comments:
Post a Comment