Klabu ya Arsenal imemtangaza kocha wa zamani wa PSG na Sevilla, Unai Emery kuwa kocha mpya atakayerithi mikoba iliyoachwa na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Arsene Wenger ambaye alitangaza kustaafu soka.
Kocha huyo anatajwa kumfukuzia nyota na winga wa Chelsea, Kanedy ambaye alitolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Newcastle alioitumikia kuanzia mwezi Januari mwaka huu.
Unai Emery anatajwa kumfukuzia winga huyo raia wa Brazil ambaye aliifungia Newcastle magoli mawili na kutengeneza mengine mawili katika kipindi alichoichezea kwa mkopo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.
Chelsea ilimnasa nyota huyo kutoka klabu ya Fluminense ya nchini Brazil ambapo huko alisajiliwa kwa dau la paundi milioni 6 lakini kusajiliwa kwa Emerson Palmieri kutoka As Roma kunatajwa kuwa kikwazo kwa nyota huyo kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha Chelsea ambapo kwa nafasi anayocheza imekua ikitumika sana na Marcos Alonso.
No comments:
Post a Comment