Klabu ya Chelsea imepanga kumtumia mshambuliaji wake raia wa Ubelgiji ili kumnasa winga wa Borrusia Dortmund raia wa Marekani, Christian Pulisic.
Borrusia Dortmund inatajwa kuvutiwa na ubora wa Batshuayi ambaye aliungana na klabu hiyo kwa mkopo kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kabla ya kupata majeraha yaliyomfanya kuwa nje na kushindwa kumalizia msimu kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga.
Dortmund inatajwa kufanya mawasiliano na Chelsea ili kumnasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 24 ambapo dau lililotajwa mwanzoni kumhusu mchezaji huyo lilikua ni paundi milioni 50 lakini Chelsea inatajwa kuvutiwa na winga wa klabu hiyo, Christian Pulisic na kwa taarifa zilizopo ni kwamba Chelsea inataka kumtumia Batshuayi ili kumpata Pulisic kwa kulazimisha kufanyika kwa mabadilishano.
No comments:
Post a Comment