Nyota wa Chelsea, N'Golo Kante ambaye kwasasa yupo pamoja na kikosi cha timu yake ya taifa ya Ufaransa amezua kituko huko nchini Ufaransa akiwa pamoja na wachezaji wa kikosi cha timu hiyo inayofundishwa na kocha Didier Deschamps.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alihusika kwenye kikosi cha wachezaji 23 watakaoiongoza timu hiyo kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2018 itakayofanyika huko nchini Urusi ambapo wachezaji hao walitakiwa kupiga picha ya pamoja ambapo kwenye picha hizo ilionekana kuwa kituko kwa Kante ambapo ufupi wake ulimfanya asionekane kwenye moja ya picha ambapo alizibwa na Paul Pogba.
Kante mwenye urefu wa mita 1.68 alizibwa kwenye picha hiyo na Paul Pogba ambaye kiumbo ni mrefu kuliko Kante akiwa na urefu wa mita 1.91 na kumfanya Kante asionekane kwenye picha hiyo huku akiishia kuonekana sehemu fupi ya mwili wake.
Tukio hili la Kante kutoonekana kwenye picha hiyo limezua gumzo kwenye magazeti mengi barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment