Usiku wa jana kumechezeka mchezo mmoja wa kirafiki unaowahusisha nyota wa Chelsea kwenye timu ya taifa ya Ubelgiji ambao ni maalumu kwa ajili ya kujinoa au kujiweka sawa kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Urusi kushiriki michuano ya Kombe la Dunia itakayoanza siku kadhaa zijazo.
Ubelgiji imemcheza mchezo huo wa kirafiki hapo jana na kufanikiwa kuibamiza Costa Rica jumla ya mabao 4-1 huku mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi akifunga goli la kukamilisha ushindi huo dakika chache baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba.
Lakini katika mchezo huo, nyota wa Chelsea, Eden Hazard alitolewa katika dakika ya 70' akiwa na maumivu hali iliyoleta hofu kwamba je ataweza kuwa sawa kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya Kombe la Dunia?
Hatimaye mara baada ya mchezo, kocha wa timu hiyo, Roberto Martinez alitoa maelezo akisema nyota huyo atakuwa sawa na atakuwepo Russia kushiriki michuano hiyo mikubwa duniani.
No comments:
Post a Comment