Kuna taarifa imeripotiwa na tovuti ya habari za michezo, tovuti ya Goal.com ambayo imeripoti kwamba Chelsea imepewa ofa ya paundi milioni 100 ili kumuuza nyota wake N'Golo Kante kwa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa.
Klabu hiyo ambayo ni mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 wamekuwa wakitajwa kuvutiwa na uwezo aliokuwa nao nyota huyo raia wa Ufaransa na ipo tayari kutoa fungu hilo litakalomfanya kuwa kiungo mkabaji ghali zaidi duniani.
Chelsea inatajwa kuweza kukubali ofa hiyo huku ikijipanga kumfukuzia kiungo mwengine raia wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Olympique Marseille, Tanguay Ndombele.
Chelsea inatajwa kumfukuzia kiungo huyo mwenye miaka 21 kama sehemu ya kuziba pengo la Kante ambaye alishinda tunzo ya mchezaji bora raia wa Ufaransa anayecheza nje ya ligi kuu nchini kwao akiwashinda nyota wengine kama Antoinne Griezman wa Atletico Madrid, Paul Pogba wa Man utd na Karim Benzema wa Real Madrid.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment