Leo nilikuletea habari kuhusu klabu ya soka ya nchini Ufaransa, PSG imetoa ofa kwa klabu ya Chelsea ikitaka kumsajili N'Golo Kante kwa dau la paundi milioni 100 na nikakutaarifu kwamba Chelsea inamfukuzia nyota kutoka Olympique Lyon ili aje kuziba pengo la nyota huyo.
Sasa je Chelsea ifanye nini ili kumshawishi Ndombele atue klabuni hapo?
Taarifa zimeripotiwa kwamba ili Chelsea ifanikiwe kumnasa nyota huyo anayeitwa Tanguy Ndombele mwenye miaka 21 anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji basi ni lazima ikubali kuachana na mmojawapo kati ya N'Golo Kante anayetakiwa na PSG au Tiemoue Bakayoko ambao wote wanacheza nafasi ya kiungo wa mkabaji.
Kumuuza mmojawapo kati ya hao kutamshawishi nyota huyo anayetakiwa na klabu nyingi barani Ulaya akubali kuvaa jezi za Chelsea msimu ujao.
Lakini pia taarifa hiyo inadai kama ikishindwa kuachana na nyota hao basi ichague mwengine wa kuachana nae kati ya Danny Drinkwater au Cesc Fabregas.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment