Kituo kimoja cha radio nchini Italia, Tele Radio Station kimemnukuu Wakala wa mlinda mlango wa klabu ya soka ya As Roma ya Italia pamoja na timu ya taifa ya Brazil, Allison Becker kuwa club ya Chelsea pamoja na Liverpool ni mojawapo ya club za England zinazo hitaji huduma za mlinda mlango huyo namba moja wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Roma
Taarifa hizo za Chelsea kumuhitaji mlinda mlango huyo zimeibuka kwa kasi baada ya mlinda mlango wa sasa wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji kutamka kua anatamani kuishi karibu na famillia yake inasadikika mke wake pamoja na mtoto wake wanaishi katika nchi ya Hispania na klabu inayo muhitaji ni Real Madrid
Ukiwa kama mdau mkubwa wa soka je Allison Becker ni mlinda mlango sahihi wakuziba pengo la Thibaut Courtois pale Chelsea? Toa maoni yako hapo chini
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment