Willian atoa majibu kuhusu kutaka kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Willian atoa majibu kuhusu kutaka kuondoka Chelsea

Share This

“Hapana, sio kweli. Mimi najiandaa kurejea London, msiamini kinachoandikwa” alisema Willian Borges alipoulizwa kuhusu taarifa zinazoenezwa kwamba nyota huyo analazimisha kuondoka Chelsea

Nyota huyo raia wa Brazil amekuwa akihusishwa mara kadhaa kulazimisha kuondoka klabuni Chelsea huku klabu ya Barcelona ikitajwa kumfukuzia mwanzoni kabla ya jana kuripotiwa kwamba klabu ya Real Madrid ipo tayari kutoa paundi milioni 100 ili kumnasa nyota huyo pamoja na mlinda mlango, Thibaut Courtois.

Willian mwenye miaka 29 alishinda tunzo ya mchezaji bora kwa wachezaji klabuni Chelsea pamoja na tunzo ya goli bora la mwaka klabuni hapo mwezi May mwaka huu.

No comments:

Post a Comment