Chelsea kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya Juventus - Darajani 1905

Chelsea kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya Juventus

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women inayosimamiwa na kocha Emma Hayes ambaye anawania tunzo ya kocha bora wa mwaka kwa soka la wanawake inayotolewa na chama cha soka Duniani, FIFA itashuka uwanjani usiku wa leo kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki ili kujiandaa na msimu mpya ambapo itacheza dhidi ya Juventus.

Chelsea FC Women ndiyo itakuwa mwenyeji katika mchezo huo ambapo itaikaribisha Juventus Ladies kwenye uwanja wa Kingsmeadow huko nchini Uingereza.

Usisahau gwiji wa soka wa Chelsea FC Women, Eniola Aluko alijiunga na klabu ya Juventus Ladies na kuna uwezekano akacheza kwenye mchezo wa leo akicheza dhidi ya klabu yake ya zamani.

No comments:

Post a Comment